Proverbs 7:7-23

7 aNiliona miongoni mwa wajinga,
nikagundua miongoni mwa wanaume vijana,
kijana asiye na akili.
8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake,
akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9 bwakati wa machweo, jua likipungua nuru yake,
giza la usiku lilipokuwa likiingia.

10 cNdipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,
hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11 d(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,
miguu yake haitulii nyumbani;
12 emara kwenye barabara za mji,
mara kwenye viwanja vikubwa,
kwenye kila pembe huvizia.)
13 fHuyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,
na kwa uso usio na haya akamwambia:

14 g“Nina sadaka za amani nyumbani;
leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;
nimekutafuta na nimekupata!
16 hNimetandika kitanda changu
kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17 iNimetia manukato kitanda changu
kwa manemane, udi na mdalasini.
18 jNjoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;
tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19Mume wangu hayupo nyumbani;
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha
na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

21 kKwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;
alimshawishi kwa maneno yake laini.
22 lMara huyo kijana alimfuata yule mwanamke
kama fahali aendaye machinjoni,
kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23 mmpaka mshale umchome ini lake,
kama ndege anayenaswa kwenye mtego,
bila kujua itamgharimu maisha yake.
Copyright information for SwhNEN